Wadau wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli wameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa usimamizi mzuri inaoufanya katika kuhakikisha Watanzania wanapewa vipaumbele vya ajira katika miradi mbalimbali inayoendelea kwenye shughuli hizo.
Pongezi hizi zinakuja baada ya Mamlaka kuhakikisha wafanyakazi wa kigeni kwenye nafasi mbalimbali katika mradi wa ukarabati wa visima Songo Songo wanaondolewa na nafasi zao kuchukuliwa na Watanzania, hususani zile ambazo hazihitaji ujuzi wa juu.
Akitoa taarifa hiyo wakati wa kikao baina ya Mamlaka na wadau kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Mshauri wa Sheria wa Kampuni ya Exalo SA ambayo ndiye Mkandarasi wa ukarabati huo, Bi. Lightness Mmbaga alieleza kuwa kuanzia Februari 2022 wafanyakazi wa kigeni wa nafasi za ‘roustabouts’ wataondoka kwenye mradi huo na nafasi hizo zote kuchukuliwa na wazawa.
Aliongeza kuwa kwasasa katika mradi huo kuna jumla ya wazawa 29 na raia wa kigeni 24, huku wafanyakazi wa nafasi za ‘floormen’ (5), ‘derrickmen’ (2) na ‘assistant driller’ (1) wakiingia kwenye kundi la wachimbaji (drillers) kuanzia Februari 1.
Naye Afisa wa masuala ya ushiriki wa wazawa (local content) kutoka kampuni ya PanAfrican Energy Ltd ambayo ndiyo mwendeshaji wa kitalu cha Songo Songo, Bi. Rehema Shija ameipongeza PURA kwa kufuatilia kwa ukaribu masuala yote hususani yahusuyo ajira kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ili Watanzania wapate kipaumbele kwa nafasi zilizopo.
“Hii inatufanya sisi waendeshaji wa kitalu kuendelea kufatilia wakandarasi ambao tunawapa tenda za shughuli mbalimbali za miradi kuhakikisha wanafuata sheria na kanuni za ushiriki wa Watanzania kwenye shughuli za mkondo wa juu wa petroli,” aliongeza.
Kwa upande wake mwanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Mafuta na Gesi (OGAWOGA) Bw. Salim R. Sultan alieleza kuwa wamefurahia hatua hiyo ya Exalo kuweka Watanzania kwenye kazi zilizokuwa zinafanywa na raia wa kigeni na kwamba hiyo ni changamoto kubwa kwa wazawa kuonesha uwezo wao katika utendaji kazi.
“Nafasi hizi za kazi ni fursa kwetu Watanzania kuonesha uwezo wetu na uzoefu wa kazi kwenye sekta hii, tunaamini nafasi hizi zitaendelea kuongezeka kwa wazawa ili kuiletea tija nchi yetu,” alifafanua.
Indonesian President Prabowo Subianto and Tanzanian President Samia Suluhu Hassan met in Brazil to discuss cooperation in energy, oil, and gas sectors. Both leaders agreed to deepen ties, focusing on trade, investment, and human resource development.
4 days, 23 hours
President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Samia Suluhu Hassan, swearing in Dr. James Peter Mataragio as the Deputy Permanent Secretary of the Ministry of Energy at a ceremony held at state house Tunguu, Zanzibar, on March 5, 2024.
8 months, 3 weeks
The 16th meeting of the East African Community (EAC) Energy Sectoral Council of Ministers, which started on February 12, 2024 at the Community's Headquarters in Arusha, has been concluded on February 14 2024.
9 months, 1 week
TANESCO to Construct Largest Solar Power Plant in Kishapu, Shinyanga Region
1 year, 5 months
The German Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ) is committing €112 million to support Kenya in the development of renewable energy and green hydrogen.
1 year, 11 months
Naibu waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato amewataka wananchi wa Kata ya Ubaruku Mbarali mkoani Mbeya kutoingiza mifugo kwenye vyanzo vya maji badala yake wavitunze ili visaidie katika upatikanaji wa nishati ya umeme nchini.
2 years
Wizara ya Nishati imeandaa Mjadala Mkubwa wa Kitaifa kuhusu nishati safi ya kupikia
2 years, 1 month
WAZIRI MAKAMBA AWAASA WABUNGE WANAWAKE KUHAMASISHA NISHATI BORA YA KUPIKIA
2 years, 2 months
WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA MABALOZI WA UINGEREZA, SINGAPORE
2 years, 2 months
TANZANIA NA OMAN KUSHIRIKIANA KUKUZA SEKTA YA NISHATI
2 years, 3 months
EWURA GCC YATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA RELI YA SGR
2 years, 4 months
EWURA imetoa mafunzo ya udhibiti kwa baadhi ya wafanyakazi wake ili kuwajengea uelewa wa misingi ya shughuli za udhibiti.
2 years, 6 months
Visima vya nishati ya Jotoardhi kuanza kuchorongwa Songwe
2 years, 7 months
Naibu Katibu Nishati akagua miundombinu ya Gesi Songosongo
2 years, 7 months
Waziri Makamba akutana na ujumbe wa Benki ya Dunia
2 years, 7 months
EWURA yakusanya maoni juu ya marekebisho ya bei za umeme kwa wananchi wa Visiwa vya Ukerewe.
2 years, 8 months
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeondoa Tozo ya Shilingi 100 kwa kila lita ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa
2 years, 8 months
Wizara ya Nishati na kampuni ya DP World ya Dubai zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania
2 years, 8 months
Mkuu wa Mkoa Mara, Mheshimiwa Ally Hapi, ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kusambaza majina ya mafundi umeme kuanzia katika ofisi za Kata
2 years, 9 months
KATIBU MKUU NISHATI ATAKA WIZARA YA NISHATI IWE KITOVU CHA UFANISI KATIBU
2 years, 9 months
EWURA KANDA YA ZIWA YATOA SEMINA KWA WADAU WA SEKTA NDOGO YAMAFUTA YA PETROLI WA MKOA WA MWANZA
2 years, 9 months
BEI YA MAFUTA YA PETROLI YASHUKA
2 years, 9 months
EWURA YAWAONGEZEA UJUZI MAMLAKA YA UDHIBITI WA NISHATI YA MALAWI MERA
2 years, 9 months
Waziri wa Nishati, Mh. January Yusuph Makamba ametoa wito kwa serikali ya India na wawekezaji wa nchini humo kutembelea nchini Tanzania ili kutazama fursa zinazopatikana kwenye maeneo mbalimbali ya sekta ya nishati.
2 years, 10 months
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba ameanzisha majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa gesi ya kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG) baina ya Serikali na Kampuni za Shell Tanzania ambao ni wawekezaji katika vitalu namba 1 na 4 na Equinor ambao ni wawekezaji katika kitalu namba 2
2 years, 11 months