Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amewaasa Wabunge Wanawake nchini kutoa elimu kwa wananchi kuhusu nishati bora ya kupikia ili kuweza kulisaidia Taifa kuepukana na Matumizi ya Nishati isiyo salama.
Alitoa Wito huo Septemba 22, 2022 wakati wa semina maalum ya kuwajengea uwezo Wabunge Wanawake kuhusu nishati bora ya kupikia vijijini iliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri Makamba aliwasihi Wabunge hasa wanawake wahakikishe wanaweka mikakati bora katika majimbo yao kama kutoa elimu juu ya Matumizi sahihi ya nishati ili kuweza kuokoa maisha ya wanawake na watu wote wanaotumia muda mwingi jikoni ambapo alitanabaisha kuwa, saa moja ya kutumia kuni ni sawa na kuvuta sigara mia tatu ambazo zinasababisha madhara makubwa ya kiafya.
“Kila Mbunge hasa nyie mama zetu tuhakikishe katika maeneo yetu tunawapa elimu ya kutosha Wananchi ambao bado hawajanufaika na matumizi sahihi ya nishati mbadala kwa sababu moshi wa kuni na mkaa hauna tofauti na yule anayevuta sigara mia tatu kwa siku kwa sababu zote zinawaletea madhara makubwa kwenye afya zao na kuharakisha vifo vyao na hata kupelekea tatizo la mimba zinazoishia katikati kama watoto kuzaliwa njiti au mimba kutoka kabla ya wakati.”Alisisitiza
Alisema Serikali imeamua kulibeba jambo hilo la uwepo wa nishati bora ya kupikia kwa ukubwa wake ili kubadilisha hali ya maisha ya wakina Mama kwa kuwaletea nishati mbadala na pia kuweza kuweka usawa kati ya walionacho na wasionacho.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Edson Ngabo alisema kuwa nishati bora ya kupikia ikiwemo matumizi ya majiko ya gesi itakapotumika kikamilifu na kwa upana mkubwa sehemu mbalimbali nchini, itasaidia kuondokana na magonjwa yanayotokana na kutumia nishati isiyo salama.
Kenya's KenGen signed a KSh 250 million deal with Eswatini to assess geothermal potential, reinforcing its role as Africa’s geothermal leader. The project supports Eswatini’s renewable energy goals while diversifying KenGen’s revenue and advancing clean energy solutions.
1 week, 4 days
Indonesian President Prabowo Subianto and Tanzanian President Samia Suluhu Hassan met in Brazil to discuss cooperation in energy, oil, and gas sectors. Both leaders agreed to deepen ties, focusing on trade, investment, and human resource development.
3 weeks, 4 days
President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Samia Suluhu Hassan, swearing in Dr. James Peter Mataragio as the Deputy Permanent Secretary of the Ministry of Energy at a ceremony held at state house Tunguu, Zanzibar, on March 5, 2024.
9 months, 1 week
The 16th meeting of the East African Community (EAC) Energy Sectoral Council of Ministers, which started on February 12, 2024 at the Community's Headquarters in Arusha, has been concluded on February 14 2024.
9 months, 4 weeks
TANESCO to Construct Largest Solar Power Plant in Kishapu, Shinyanga Region
1 year, 6 months
The German Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ) is committing €112 million to support Kenya in the development of renewable energy and green hydrogen.
1 year, 11 months
Naibu waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato amewataka wananchi wa Kata ya Ubaruku Mbarali mkoani Mbeya kutoingiza mifugo kwenye vyanzo vya maji badala yake wavitunze ili visaidie katika upatikanaji wa nishati ya umeme nchini.
2 years, 1 month
Wizara ya Nishati imeandaa Mjadala Mkubwa wa Kitaifa kuhusu nishati safi ya kupikia
2 years, 1 month
WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA MABALOZI WA UINGEREZA, SINGAPORE
2 years, 3 months
TANZANIA NA OMAN KUSHIRIKIANA KUKUZA SEKTA YA NISHATI
2 years, 4 months
EWURA GCC YATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA RELI YA SGR
2 years, 5 months
EWURA imetoa mafunzo ya udhibiti kwa baadhi ya wafanyakazi wake ili kuwajengea uelewa wa misingi ya shughuli za udhibiti.
2 years, 7 months
Visima vya nishati ya Jotoardhi kuanza kuchorongwa Songwe
2 years, 8 months
Naibu Katibu Nishati akagua miundombinu ya Gesi Songosongo
2 years, 8 months
Waziri Makamba akutana na ujumbe wa Benki ya Dunia
2 years, 8 months
EWURA yakusanya maoni juu ya marekebisho ya bei za umeme kwa wananchi wa Visiwa vya Ukerewe.
2 years, 9 months
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeondoa Tozo ya Shilingi 100 kwa kila lita ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa
2 years, 9 months
Wizara ya Nishati na kampuni ya DP World ya Dubai zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania
2 years, 9 months
Mkuu wa Mkoa Mara, Mheshimiwa Ally Hapi, ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kusambaza majina ya mafundi umeme kuanzia katika ofisi za Kata
2 years, 10 months
KATIBU MKUU NISHATI ATAKA WIZARA YA NISHATI IWE KITOVU CHA UFANISI KATIBU
2 years, 10 months
EWURA KANDA YA ZIWA YATOA SEMINA KWA WADAU WA SEKTA NDOGO YAMAFUTA YA PETROLI WA MKOA WA MWANZA
2 years, 10 months
BEI YA MAFUTA YA PETROLI YASHUKA
2 years, 10 months
EWURA YAWAONGEZEA UJUZI MAMLAKA YA UDHIBITI WA NISHATI YA MALAWI MERA
2 years, 10 months
Wadau wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli wameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa usimamizi mzuri inaoufanya katika kuhakikisha Watanzania wanapewa vipaumbele vya ajira katika miradi mbalimbali inayoendelea kwenye shughuli hizo
2 years, 10 months
Waziri wa Nishati, Mh. January Yusuph Makamba ametoa wito kwa serikali ya India na wawekezaji wa nchini humo kutembelea nchini Tanzania ili kutazama fursa zinazopatikana kwenye maeneo mbalimbali ya sekta ya nishati.
2 years, 11 months
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba ameanzisha majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa gesi ya kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG) baina ya Serikali na Kampuni za Shell Tanzania ambao ni wawekezaji katika vitalu namba 1 na 4 na Equinor ambao ni wawekezaji katika kitalu namba 2
3 years