TANZANIA NA OMAN KUSHIRIKIANA KUKUZA SEKTA YA NISHATI
Waziri wa Nishati Mhe.January Makamba amekutana na Mhe. Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Saud Hilal Al Shidhani na kuzungumzia fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika sekta ya mafuta na gesi hususani katika miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa nchini.Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ndogo ya Wizara ya Nishati Jijini Dar es Salaam leo tarehe 16 Agosti,2022 na yalijikita katika kuzungumzia makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan yaliyofanyika nchini Oman Juni, 2022.Kupitia Mazungumzo hayo Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) litashirikiana na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Oman (OQ) kufanya biashara ya mafuta ya jumla (fuel supply), kujenga vituo vikubwa vya gesi za mitungi (LPG) na kushirikiana na Kampuni Tanzu ya TPDC (TANOIL) ili kufanya biashara ya rejareja ya mafuta.Halikadhalika, wataalamu kutoka nchini Oman kuendelea kuja nchini Tanzania kuangalia miundombinu ya Bandari na kutazama maeneo ya kuwekeza kwenye miundombinu ya kupokea, kushusha, kuhifadhi na kutoa mafuta katika Bandari na Ghala za dhamana ya forodha pamoja na kubadilishana uzoefu na Tanzania.Waziri wa Makamba wakati wa mazungumzo hayo amesema Tanzania inatafuta Washirika wa kimkakati ambao watashirikiana na TPDC katika kutafuta mafuta na gesi katika vitalu vilivyopo ili kuchochea ukuaji wa viwanda na kuongeza ukuaji wa uchumi nchini hususan katika miradi ya kimkakati ukiwemo wa Mwalimu Julius Nyerere.Akizungumza katika Mkutano huo Mhe. Balozi Saud Hilal Al Shidhani pamoja na kutoa salaam za Rais wa Oman amemshukuru Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa utayari wake wa kushirikiana na Oman katika kuendeleza sekta ya nishati.Aidha, amesema Oman ina ujuzi mkubwa katika masuala ya mafuta hivyo amemhakikishia Waziri Makamba kuwa watashirikiana vyema katika kukuza sekta hiyo nchini Tanzania.
Kenya's KenGen signed a KSh 250 million deal with Eswatini to assess geothermal potential, reinforcing its role as Africa’s geothermal leader. The project supports Eswatini’s renewable energy goals while diversifying KenGen’s revenue and advancing clean energy solutions.
1 week, 4 days
Indonesian President Prabowo Subianto and Tanzanian President Samia Suluhu Hassan met in Brazil to discuss cooperation in energy, oil, and gas sectors. Both leaders agreed to deepen ties, focusing on trade, investment, and human resource development.
3 weeks, 4 days
President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Samia Suluhu Hassan, swearing in Dr. James Peter Mataragio as the Deputy Permanent Secretary of the Ministry of Energy at a ceremony held at state house Tunguu, Zanzibar, on March 5, 2024.
9 months, 1 week
The 16th meeting of the East African Community (EAC) Energy Sectoral Council of Ministers, which started on February 12, 2024 at the Community's Headquarters in Arusha, has been concluded on February 14 2024.
9 months, 4 weeks
TANESCO to Construct Largest Solar Power Plant in Kishapu, Shinyanga Region
1 year, 6 months
The German Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ) is committing €112 million to support Kenya in the development of renewable energy and green hydrogen.
1 year, 11 months
Naibu waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato amewataka wananchi wa Kata ya Ubaruku Mbarali mkoani Mbeya kutoingiza mifugo kwenye vyanzo vya maji badala yake wavitunze ili visaidie katika upatikanaji wa nishati ya umeme nchini.
2 years, 1 month
Wizara ya Nishati imeandaa Mjadala Mkubwa wa Kitaifa kuhusu nishati safi ya kupikia
2 years, 1 month
WAZIRI MAKAMBA AWAASA WABUNGE WANAWAKE KUHAMASISHA NISHATI BORA YA KUPIKIA
2 years, 2 months
WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA MABALOZI WA UINGEREZA, SINGAPORE
2 years, 3 months
EWURA GCC YATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA RELI YA SGR
2 years, 5 months
EWURA imetoa mafunzo ya udhibiti kwa baadhi ya wafanyakazi wake ili kuwajengea uelewa wa misingi ya shughuli za udhibiti.
2 years, 7 months
Visima vya nishati ya Jotoardhi kuanza kuchorongwa Songwe
2 years, 8 months
Naibu Katibu Nishati akagua miundombinu ya Gesi Songosongo
2 years, 8 months
Waziri Makamba akutana na ujumbe wa Benki ya Dunia
2 years, 8 months
EWURA yakusanya maoni juu ya marekebisho ya bei za umeme kwa wananchi wa Visiwa vya Ukerewe.
2 years, 9 months
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeondoa Tozo ya Shilingi 100 kwa kila lita ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa
2 years, 9 months
Wizara ya Nishati na kampuni ya DP World ya Dubai zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania
2 years, 9 months
Mkuu wa Mkoa Mara, Mheshimiwa Ally Hapi, ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kusambaza majina ya mafundi umeme kuanzia katika ofisi za Kata
2 years, 10 months
KATIBU MKUU NISHATI ATAKA WIZARA YA NISHATI IWE KITOVU CHA UFANISI KATIBU
2 years, 10 months
EWURA KANDA YA ZIWA YATOA SEMINA KWA WADAU WA SEKTA NDOGO YAMAFUTA YA PETROLI WA MKOA WA MWANZA
2 years, 10 months
BEI YA MAFUTA YA PETROLI YASHUKA
2 years, 10 months
EWURA YAWAONGEZEA UJUZI MAMLAKA YA UDHIBITI WA NISHATI YA MALAWI MERA
2 years, 10 months
Wadau wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli wameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa usimamizi mzuri inaoufanya katika kuhakikisha Watanzania wanapewa vipaumbele vya ajira katika miradi mbalimbali inayoendelea kwenye shughuli hizo
2 years, 10 months
Waziri wa Nishati, Mh. January Yusuph Makamba ametoa wito kwa serikali ya India na wawekezaji wa nchini humo kutembelea nchini Tanzania ili kutazama fursa zinazopatikana kwenye maeneo mbalimbali ya sekta ya nishati.
2 years, 11 months
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba ameanzisha majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa gesi ya kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG) baina ya Serikali na Kampuni za Shell Tanzania ambao ni wawekezaji katika vitalu namba 1 na 4 na Equinor ambao ni wawekezaji katika kitalu namba 2
3 years