Energy Policy & Regulation

WAZIRI MAKAMBA ATOA WITO INDIA KUWEKEZA SEKTA YA NISHATI

3 years, 1 month
Anakletus John

Waziri wa Nishati, Mh. January Yusuph Makamba ametoa wito kwa serikali ya India na wawekezaji wa nchini humo kutembelea nchini Tanzania ili kutazama fursa zinazopatikana kwenye maeneo mbalimbali ya sekta ya nishati ikiwa ni pamoja na zile za kitalu cha Mnazi Bay North ili kufanya uwekezaji.

Waziri Makamba ameyasema hayo, Jumatano, Januari 5, 2022 alipokutana na Balozi wa India nchini Tanzania Mh. Binaya S. Pradhan katika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalilenga kujadili ushirikiano kwa kisekta baina ya Tanzania na India.

Alieleza kuwa zipo fursa za uwekezaji kwenye kitalu hicho ambazo zinahitaji uwekezaji wa haraka na hivyo wafanyabiashara na wawekezaji hao wajitokeze ili kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) katika kuzitumia fursa husika.

Vivyohivyo, alisema zipo fursa za uwekezaji kwenye miradi ya nishati ya jua na ujenzi wa maghala ya kutunzia mafuta ambayo ni hitaji kubwa kwa Tanzania na inaweza kutumika kimkakati kusambaza mafuta katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

“Nawakaribisha sana wawekezaji wa India kuwekeza katika fursa za maghala ya mafuta kwa kushirikiana na kampuni ya kuhifadhi mafuta (Tiper) kwa kutumia miundombinu yake ambayo tayari imeshajengwa, kikubwa ikiwa ni kuzingatia uboreshaji wa miundombinu hiyo,” amefafanua Waziri Makamba.

Kwa upande wake, Balozi Pradhan alisema Serikali ya India itaendelea kushirikiana na Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwahimiza wafanyabiashara na wawekezaji wake kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana nchini.

Alieleza kuwa kwa sasa Serikali hiyo inatazamia kuwekeza nchini Tanzania kwenye eneo la maghala ya mazao ya petroli, fursa zinazotokana na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani Tanzania (EACOP) pamoja na miradi ya umeme wa jua (solar) ukiwemo ule wa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

“Serikali ya India kwa kushirikiana na sekta binafsi imejipanga kuendelea kufanya uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali ya kimaendeleo duniani kote, ikiwemo nchini Tanzania,” aliongeza.


Comments

Add comment

Related Post

Energy Policy & Regulation

KENYA INVESTS KSH 250M IN ESWATINI FOR GEOTHERMAL ENERGY DEAL.

Kenya's KenGen signed a KSh 250 million deal with Eswatini to assess geothermal potential, reinforcing its role as Africa’s geothermal leader. The project supports Eswatini’s renewable energy goals while diversifying KenGen’s revenue and advancing clean energy solutions.

2 months, 2 weeks

Energy Policy & Regulation

INDONESIA, TANZANIA DISCUSS ENERGY, GAS COOPERATION IN BRAZIL.

Indonesian President Prabowo Subianto and Tanzanian President Samia Suluhu Hassan met in Brazil to discuss cooperation in energy, oil, and gas sectors. Both leaders agreed to deepen ties, focusing on trade, investment, and human resource development.

3 months

Energy Policy & Regulation

TANZANIA: PRESIDENT SAMIA SWEARS IN DEPUTY SECRETARY.

President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Samia Suluhu Hassan, swearing in Dr. James Peter Mataragio as the Deputy Permanent Secretary of the Ministry of Energy at a ceremony held at state house Tunguu, Zanzibar, on March 5, 2024.

11 months, 3 weeks

Energy Policy & Regulation

TANZANIA: THE 16TH MEETING OF EAST-AFRICA ENERGY SECTORAL MINISTRIES CONCLUDED IN ARUSHA.

The 16th meeting of the East African Community (EAC) Energy Sectoral Council of Ministers, which started on February 12, 2024 at the Community's Headquarters in Arusha, has been concluded on February 14 2024.

1 year

Energy Policy & Regulation

SHINYANGA: Tanesco to Construct Largest Solar Power Plant in Kishapu, Shinyanga Region

TANESCO to Construct Largest Solar Power Plant in Kishapu, Shinyanga Region

1 year, 8 months

Energy Policy & Regulation

KENYA: GERMAN COMMITTING €112 MILLION TO SUPPORT ENERGY

The German Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ) is committing €112 million to support Kenya in the development of renewable energy and green hydrogen.

2 years, 1 month

Energy Policy & Regulation

Naibu Waziri Nishati Ahimiza Kutunza Vyanzo Vya Maji Vya Kuzalisha Umeme

Naibu waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato amewataka wananchi wa Kata ya Ubaruku Mbarali mkoani Mbeya kutoingiza mifugo kwenye vyanzo vya maji badala yake wavitunze ili visaidie katika upatikanaji wa nishati ya umeme nchini.

2 years, 3 months

Energy Policy & Regulation

MJADALA WA KITAIFA KUHUSU NISHATI SAFI

Wizara ya Nishati imeandaa Mjadala Mkubwa wa Kitaifa kuhusu nishati safi ya kupikia

2 years, 3 months

Energy Policy & Regulation

MAKAMBA AWAASA WABUNGE WANAWAKE KUHAMASISHA NISHATI BORA YA KUPIKIA

WAZIRI MAKAMBA AWAASA WABUNGE WANAWAKE KUHAMASISHA NISHATI BORA YA KUPIKIA

2 years, 5 months

Energy Policy & Regulation

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA MABALOZI WA UINGEREZA, SINGAPORE

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA MABALOZI WA UINGEREZA, SINGAPORE

2 years, 5 months

Energy Policy & Regulation

TANZANIA NA OMAN KUSHIRIKIANA KUKUZA SEKTA YA NISHATI

TANZANIA NA OMAN KUSHIRIKIANA KUKUZA SEKTA YA NISHATI

2 years, 6 months

Energy Policy & Regulation

EWURA GCC YATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA RELI YA SGR

EWURA GCC YATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA RELI YA SGR

2 years, 7 months

Energy Policy & Regulation

EWURA YAWANOA WAFANYAKAZI WAKE

EWURA imetoa mafunzo ya udhibiti kwa baadhi ya wafanyakazi wake ili kuwajengea uelewa wa misingi ya shughuli za udhibiti.

2 years, 9 months

Energy Policy & Regulation

Visima  Vya Nishati Ya Jotoardhi Kuanza Kuchorongwa Songwe

Visima  vya nishati ya Jotoardhi kuanza kuchorongwa Songwe

2 years, 10 months

Energy Policy & Regulation

Naibu Katibu Nishati Akagua Miundombinu Ya Gesi Songosongo

Naibu Katibu Nishati akagua miundombinu ya Gesi Songosongo

2 years, 10 months

Energy Policy & Regulation

Waziri Makamba Akutana Na Ujumbe wa Benki ya Dunia

Waziri Makamba akutana na ujumbe wa Benki ya Dunia

2 years, 10 months

Energy Policy & Regulation

EWURA YAKUSANYA MAONI JUU YA MAREKEBISHO YA BEI ZA UMEME

EWURA yakusanya maoni juu ya marekebisho ya bei za umeme kwa wananchi wa Visiwa vya Ukerewe.

2 years, 11 months

Energy Policy & Regulation

SERIKALI YAONDOA TOZO YA MAFUTA

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeondoa Tozo ya Shilingi 100 kwa kila lita ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa

2 years, 11 months

Energy Policy & Regulation

TANZANIA NA DUBAI ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO SEKTA YA NISHATI

Wizara ya Nishati na kampuni ya DP World ya Dubai zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania

2 years, 11 months

Energy Policy & Regulation

EWURA YATAKIWA KUSAMBAZA ORODHA YA MAFUNDI UMEME KATIKA OFISI ZA KATA

Mkuu wa Mkoa Mara, Mheshimiwa Ally Hapi, ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kusambaza majina ya mafundi umeme kuanzia katika ofisi za Kata

3 years

Energy Policy & Regulation

KATIBU MKUU ATAKA WIZARA YA NISHATI IWE KITOVU CHA UFANISI

KATIBU MKUU NISHATI ATAKA WIZARA YA NISHATI IWE KITOVU CHA UFANISI KATIBU

3 years

Energy Policy & Regulation

EWURA YATOA SEMINA KWA WADAU WA SEKTA YA MAFUTA WA MWANZA

EWURA KANDA YA ZIWA YATOA SEMINA KWA WADAU WA SEKTA NDOGO YAMAFUTA YA PETROLI WA MKOA WA MWANZA

3 years

Energy Policy & Regulation

EWURA YAWAONGEZEA UJUZI MAMLAKA YA UDHIBITI YA MALAWI

EWURA YAWAONGEZEA UJUZI MAMLAKA YA UDHIBITI WA NISHATI YA MALAWI MERA

3 years

Energy Policy & Regulation

Wadau waipongeza PURA usimamizi mzuri wa ushiriki wa wazawa

Wadau wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli wameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa usimamizi mzuri inaoufanya katika kuhakikisha Watanzania wanapewa vipaumbele vya ajira katika miradi mbalimbali inayoendelea kwenye shughuli hizo

3 years

Energy Policy & Regulation

​Waziri Makamba aanzisha Majadiliano Mradi wa LNG

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba ameanzisha majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa gesi ya kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG) baina ya Serikali na Kampuni za Shell Tanzania ambao ni wawekezaji katika vitalu namba 1 na 4 na Equinor ambao ni wawekezaji katika kitalu namba 2

3 years, 2 months